Habari zenu ndugu, jamaa na rafiki zangu wa Twitter na nyote wengine mliopo duniani kote. Nawasalimu kwa jina la Muumba wa mbingu na Nchi aliyetupa afya na uzima mpaka leo hii tunaivuta pumzi yake. Napenda kuchukua muda huu kuaandikia makala hii, japo makala itakua ndefu ila naomba ndugu zangu msichoke kaaeni nami hadi mwisho naamini kuna mengi ambayo unaweza kujifunza kupitia makala hii.
Shukrani zangu
Kwanza naomba nianze na shukrani zangu kwa Mungu kunijalia moyo mnyenyekevu na msikivu na kuendelea kunilinda japo namkosea mara kwa mara kwa kutenda dhambi za makusudi na bahati mbaya na pia shukrani zangu zende kwa Wazazi wangu kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi kwa nyakati zote nilizo / ninazo pitia na kunitia moyo nisikate tamaa bila kuwasahau jamaa na rafiki zangu wote walio na mimi katika mabonde na milima, huzuni na furaha. Sina chakuwalipa ila mweyezi Mungu akawape kila mmoja haja njema ya moyo wake.
Historia ya CHAMP SOAP
Naitwa Andrew Mpambazi ni mtanzania halisi na mjasiriamali ninae tengeneza Sabuni za kuogea na kufulia ziitwazo CHAMP SOAP naimani wengi mmeshakutana nazo kama sio mitaani na madukani basi mitandaoni ama kuelezwa na jamaa zenu kuhusu sabuni hizo.
Sabuni za kuogea za Champ soap kwa sasa zimetimiza mwaka mmoja na wiki kadhaa kumbukumbu zangu zinasema nilianza rasmi kuzitengeneza mnamo mwaka Jana 2020 mwezi July. Nashukuru Mungu tena na watu wa jamii ya Twitter kwa kunipokea vizuri na kwaukubwa ambao sikuutarajia na kufanya kwa muda mfupi Champ soap kusikika kwenye masikio ya watu wengi, Hali hiyo ilipelekea kila mtu kutaka kuijaribu kujua nini kilichomo ndani ya sabuni hiyo na ubora wake.
Hali hiyo ilinipa wateja wengi sana na baada ya muda flani kupita nilikua napokea mrejesho kwa watu mbali mbali wakiipa sifa nyingi sabuni yangu watu wachache ninao wakumbuka waliowahi kunipa mrejesho wa champ soap ni dada yangu flaviana matata, kaka Gillsaint na Togolani, nimewataja hawa kwakua wengi wetu tunao tumia Twitter tunawafahamu.
Pia naishukuru #TOTbonanza kwa kuwezesha Champ soap kuwafikia wateja wengi ambao walitaka kuiona kwa ukaribu na kujiridhisha kwa macho uwepo wa Sabuni hii. Pongezi zangu zende kwa FRED KAVUSHE. Mwisho Siwezi kusahau kujishukuru Mimi pia kwa kuwaza na kufanyia kazi mawazo yangu.
Dhumuni la makala hii ni kuelezea kusitishwa kwa muda wa miezi miwili kusambaza na kuzalisha Champ soap hali iliofanya wateja na wadau wetu wengi kurudi nyuma.
Uzushi ulioikumba Champ Soap
Sabuni ya Champ ilizushiwa uzushi ya kwamba inasumu na imeua watu wengi sitaki nirudie kuelezea habari hizi maana wote mnazikumbuka mimi binafsi sitaki kukumbuka maumivu nilioyapitia na nikikumbuka machozi ya uchungu yananitiririka bila kukoma na moyo wangu kuuma sana. Nachoweza kusema ni kwamba wote waliohusika na kusambaza habari hizo za uzushi nimewasamehe ila kiukweli siwezi kusahau.
Leo kupitia ukurasa huu nitaandika nimevuka vipi hadi kufikia sasa sabuni kuruhusiwa kurudi tena sokoni ndio kuruhusiwa maana nilifungiwa kusambaza na kuzalisha.
Kwanza baada ya uzushi ule mamlaka ya kwanza kunitafuta ni TBS na ikaniamuru kupeleka vipande 6 vya sabuni ya Champ kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma hizo nakumbuka mimi nilipeleka vipande 12 na baada ya siku 14 majibu yakatoka.
Kabla majibu hayajatoka watu wa OSHA wakanitafuta wao hawakua na mambo mengi na mimi kwakua nafanyia uzalishaji wa Sabuni zangu katika kiwanda wanacho kifahamu. Niliwahi kueleza kwenye interview yangu na Dar24 kuwa niliingia mkataba na kampuni ingine ili niwe nazalishia sabuni zangu katika eneo lao kwakua bado sijawa na eneo langu. Hivyo nikamalizana na watu wa OSHA.
Baada ya siku kadhaa SIDO Kigoma wakanitafuta ikabidi kusafiri kurudi Kigoma napofanyia uzalishaji wangu nakumbuka kipindi huo uzushi unatokea nilikua Dar es Salaam, nilipofika Kigoma nikaenda kukutana nao wao walitaka kufahamu eneo ninalo fanyia uzalishaji pamoja na mkataba wa makubaliano ya uzashaji kwa ile kampuni nikafanya hayo nikamaliza.
TMDA nao hawakubaki nyuma walinitafuta ili kujua nini hasa ukweli wa hizo tuhuma nashukuru nao nikamalizana nao.
Baada ya yote hayo ikanibidi sasa nijipeleke TRA mwenye bila kuitwa ili kuulizia ninacho kifanya kama nilikua sahihi wao wakasema sipaswi kuwa na kitambulisho cha ujasiliamali kwa shughuli ninazo fanya. Wakanitengenezea TIN namba ya biashara na kuniingiza kwenye mfumo wa ulipaji Kodi pia walinikadilia kiasi cha Kodi nachotakiwa kulipa kwa mwaka na kuniamuru kulipa nami nikalipa hivyo nafurahia kuwa mlipa Kodi na nitalipa Kodi kwa maendeleo ya Taifa langu.
Baada ya kumalizana na TRA nikaelekezwa kwenda HALMASHAURI ili kukata leseni ya biashara nami nikafanya hivyo pia nashukuru Mungu hapa nilipo ninatembea na leseni ya biashara.😂😂
Watu wa mwisho kunitafuta ni watu wa mionzi ya Atomic hawa niliwekwa kwenye tuhuma nao pia kama mnakumbuka nilivyo waelekeza tukamaliza.
Sasa turudi TBS majibu yakatoka kuwa sabuni yangu imepimwa vipimo zaidi ya 8 na vyote vimetoka vizuri isipokua kimoja ndio kimezidi kidogo. (Total free alkaline) hivyo nikaamuliwa kurudi kiwandani na kutengeza sample nyengine niipeleke ili ikapimwe tena kuhakikisha hakuna kipimo kinaenda tofauti nami nikatii baada ya kutengeneza nikasafiri kuleta sample Dar es Salaam. Ukumbuke Dar es Salaam ndipo ilipo maabara kuu ya Taifa ya Tbs nikaambiwa nisubiri siku zingine 14 za majibu.
Majibu hayo yametoka tarehe 4 Agust 2021 na kusema vipimo vyote sasa vipo vizuri na wao kuniruhusu kuingiza sokoni sabuni hiyo kwa makubaliano ya kuzingatia ubora huo siku zote na pia wao wataendelea na mchakato wa kunipatia nembo ya ubora hapo baadae kidogo. Pia TBS ikaniamuru nizingatie namna sahihi ya maandishi katika Box langu la champsoap hivyo hapo baadae kidogo kutakua na mabadiriko kidogo katika Box letu la champ soap.
Hivyo kwa sasa tutamalizia Box zilizopo kwa sabuni mpya ila sabuni zijazo zitakuwa na box lenye utofauti kidogo wa maandishi tu kama tulivyo shauriwa. Naombeni tuendelee kutumia sabuni yetu na kuwa mabalozi wazuri huko duniani kote. Asante sana
Nashukuru Mungu tena na tena na watu wote mlio kuwa pamoja na mimi wakati ule mgumu. Mungu akazidi kuwabariki na kuwalinda. Na baraka zake Mungu mwenyezi ziwe pamoja nanyi siku zote za uhai wenu, na kila gumu akawafanyie wepesi, akawape moyo wa adili, hekima na busara. Kama mlivyonifaa mimi mkawafae wengine. Asanteni sana
Funzo mlilonipa walimwengu ni kubwa sana.
CHAMP SOAP FOR EVERYBODY.✊🏿
***********************************************************************************
Imeandikwa na Founder & CEO wa allottetv
Naaam masta kila hatua dua💪💪✊
ReplyDeleteChamp soap for everybody. 💪🏾💪🏾
ReplyDeleteKwa uzushi ulivyosambazwa ni vyema ukaweka wazi hivyo vyeti kama TIN, LSSENI NA TBS ili kuwaondolea shaka wateja wako
ReplyDeletePole na hongera,kuwa na moyo wa jitihada sisi vijana tunategemea ajira huko
ReplyDelete