Type Here to Get Search Results !

Ads

Vitu 6 vinavyobebwa na NIDHAMU ilikutusaidia Tufanikiwe Maishani



Nidhamu ni adabu njema kwenye familia, jeshi, hata kwenye shule. Mtu mwenye nidhamu ni mtu ambaye anafanya kazi inayofanana na ambayo ilikuwa malengo yake na jamii. hii ni maana inayopatikana katika kamusi ya wikipedia. ila leo tunaenda kuangalia maana ya neno nidhamu kutokana na herufi zinazojenga neno hili N.I.D.H.A.M.U, ungana nami katika kuzichambua.

N - (nia); unapotaka kufanya jambo lolote, jiulize je una nia gani ya kutaka kufanya jambo hilo? Na je nia ni njema au la? Kama nia si njema achana nalo.

I - (Imani); jiulize , je imani yako ya dini inaruhusu kufanya jambo hilo? na kama imani ya dini hairuhusu, achana nalo.

D -(Dhamira); dhamira yako yako inakuambia nini kuhusu jambo hilo unalotaka kulifanya? Je, inakusuta au inakukataza usilifanye? Kama inakusuta achana nalo? Hapo dhamira yako itakuwa hai.

H – (Heshima); jiulize, je hilo jambo utakalo kulifanya litakupa heshima au litakukuvunjia heshima? Kama litakuvunjia heshima usilifanyae.

A – (Akili); tumia akili yako utakapo taka kufanya jambo lolote na usifuate sana hisia zako zinavyokutuma.

M – (Maadili); jiuize, je hilo jambo unalotaka kulifanya linaendana na maadili yetu mema ya kiafrika au kitanzania? Kama liko kinyume na maadili yetu achana nalo.

U – ( utii); kuwa mtii watu wanapo kushauri mambo mema juu ya jambo unalokusudia kulifanya.yatii hayo mema uambiwayo.

kwahiyo na kutokana na huu uchambuzi mfupi inatuonesha nijinsi gani nidhamu ni muhimu katika maisha na mafanikio yetu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad

Hollywood Movies